KENYA: Mlinzi wa shule, amehukumiwa miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka 11

Mwanaume mmoja(65) mlinzi wa shule, amehukumiwa miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka 11. Alishtakiwa kwa kutenda makosa hayo ya ulawiti kuanzia December 30 na December 31, 2013. 



Mwanaume huyo alikuwa akimuita mtoto huyo mara kwa mara alipokuwa akiangalia mchezo wa mpira wa miguu katika viwanja vya shule kisha akamfanyia unyama huo katika nyumba yake. Aidha alikuwa akimtishia kumuua mtoto huyo endapo angetoa siri.