Master J amedai kuwa inamuuma mno pale ambapo anapoona washindi wa Bongo Star Search wakishindwa kufanya vizuri

Master J amedai kuwa inamuuma mno pale ambapo anapoona washindi wa Bongo Star Search wakishindwa kufanya vizuri tofauti na matarajio. Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, mtayarishaji huyo mkongwe wa muziki, amedai kuwa sababu kubwa ya washindi hao kushindwa kufanya vizuri ni vipaumbele wanavyoviwekwa baada ya kushinda.



Amedai kuwa washindi wengi walipopata fedha zao, walikuwa hawaendi kuwekeza kwenye muziki bali kuzitumia fedha hizo kutatua changamoto zao za kimaisha. “Sisi tuliassume tu kwamba ukimwezesha ataenda kujiwezesha kwenye fani hii ambayo amekuja kutuomba tumsaidie kwenye BSS. Lakini wengi wamekuwa wananidisappoint sana, wanawekeza zaidi kwenye vitu vya anasa. Kwahiyo mtu amepata milioni 50 cha kwanza anafikiria gari, wanafikiria nguo na starehe hizi za vijana,” amesema. “Hizo hela bwana unatakiwa usifanye vitu kama hivyo, unatakiwa kuiwekeza kwanza, tumekupatia mtaji, hutakiwi kula mtaji, mtaji unawekeza, pale unapopata faida ndio unabadilisha maisha yako,” aliongeza.

Master J amesisitiza kuwa alimshauri Madam Rita kuwa siku za usoni ni vyema washindi wakapewa fedha nusu na zingine zikatumika kama mtaji wa muziki wao. Hadi sasa mshindi wa BSS mwaka jana Kanumba hajaonesha kufanya vizuri kwenye muziki.

BONGO5