Kwanini Shamsa Ford anasema ajaacha Kuigiza



Ni kipindi kirefu mwigizaji Shamsa ford amekuwa kimya, baada ya kutokuonekana katika filamu ambazo zinatoka siku za hivi karibu na watu wengine wakidhani kuwa ameacha kuigiza hasa baada ya kufunga ndoa. Shamsa ford ambaye amewahi kutamba katika filamu nyingi hasa katika filamu ya BADO NATAFUTA, CHAUSIKU na nyingine nyingi katika kurasa yake ya Instagram ameyaandika haya kuhusu msimao wake kama ataendelea kwenye tasnia ya filamu.

Nimekuwa nikipokea maswali mengi SANA kutoka kwa mashabiki wangu. Wengi wao wananiuliza kama nimeacha kuigiza baada ya kuolewa. ..Naomba niwajibu mashabiki zangu..sijaacha kuigiza na very soon mtaona kazi zangu nyingi na nzuri ambazo zipo sokoni. .kwa kuanza pls msikose kuiona hiyo movie inayojulikana kwa jina la DHAMANA .Jumatatu itakuwa sokoni.