Lindi yabaini wanafunzi hewa 6,200



Mkoa wa Lindi umebaini kuwepo kwa wanafunzi hewa 6,200 katika shule za msingi na sekondari.
Wanafunzi hao hewa wameisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. milioni 38 katika miezi nane ya kwanza ya mwaka, huku Halmashauri ya Liwale na Nachingwea, zikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa za wanafunzi hao.

Takwimu hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha wakuu wa shule za sekondari na kuweka mikakati ya kuboresha elimu kilichofanyika mjini hapa juzi.#Nipashe