MKURANGA, PWANI: Jeshi la Polisi limewaua watu 4 wanaosadikiwa kuwa majambazi



Jeshi la Polisi limewaua watu 4 wanaosadikiwa kuwa majambazi katika majibizano ya risasi usiku wa kuamkia leo.  Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika mapambano hayo majambazi wengine walitoroka na watatu walifariki wakati wakikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na risasi na msako uliendelea kwa kushirikiana na wananchi.

Aidha Jeshi la Polisi lilikamata silaha aina ya Shortgun Pump Action ikiwa na risasi Tano ndani ya Magazini na nyingine 6 za Shortigun zikiwa ndani ya mfuko wa rambo pamoja na risasi nane za Pistol.