Mtanzania Thomas Ulimwengu akataa kuongeza mkataba mwingine TP Mazembe



Mtanzania Thomas Ulimwengu amemaliza mkataba na Klabu ya TP Mazembe, akataa kuongeza mkataba kwa lengo la kwenda kucheza soka Ulaya. Licha ya TP Mazembe kufanya juhudi za kutaka kumpatia mkataba mpya, Ulimwengu hakuwa tayari badala yake akasisitiza kuwa, ni muda muafaka kwake kufuata nyayo za Mbwana Samatta. Thomas Ulimwengu ambaye ameitumikia Klabu ya TP Mazembe kwa kipindi cha miaka mitano.