Mfalme wa Morocco akubali Kujenga msikiti mkubwa Dar, Uwanja wa Bil 80 Dodoma



MFALME Mohammed VI wa Morocco amekubali maombi ya Rais John Magufuli ya kujenga uwanja wa mpira mjini Dodoma ambao utakuwa mkubwa kuliko ule wa Taifa jijini Dar es Salaam sambamba na kujenga msikiti mkubwa jijini humo. Rais Magufuli aliyasema hayo Ikulu Dar es Salaam jana wakati akitoa shukrani baada ya kukutana na kiongozi huyo, aliyeambatana na wajumbe 150 ambao pamoja na mambo mengine, nchi hizo mbili zilisaini Mikataba ya Makubaliano (MoU) 21.

Akitoa taarifa fupi ya mazungumzo baina yao, Rais Magufuli alisema Mfalme Mohammed VI amekubali kujenga msikiti mkubwa jijini Dar es Salaam sambamba na kujenga uwanja wa mpira mjini Dodoma wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 80 (zaidi ya Sh bilioni 160). “Katika mazungumzo yetu, nimshukuru Mfalme Mohammed wa Morocco amekubali ombi langu la kujenga msikiti mkubwa hapa Dar es Salaam, na amekubali kwenye mji mkuu Dodoma, atajenga uwanja wa mpira utakaokuwa mkubwa kuliko wa Dar, na thamani yake ni zaidi ya Dola milioni 80,” alieleza Dk Magufuli. 


#HabariLeo