Polisi inamshikilia muuguzi wa hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uzembe uliopelekea mama kujifungua kichanga kikiwa kimefariki

Jeshi la Polisi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya linamshikilia muuguzi wa afya katika hospitali ya Wilaya ya Chunya, Patricia Kisoti, kwa kutokana na uzembe uliopekekea mama mjamzito kujifungua mtoto akiwa amekufa.



Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa muuguzi huyo Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amesema kitendo kilicho fanywa na muuguzi huyo nichakinyama na kimetia aibu sekta ya afya.

Amesema September 4, mwaka huu katika hospitali ya Wilaya ya Chunya, mjamzito huyo akiwa ameongozana na mwenzake walifika kituoni hapo usiku, wakihitaji huduma ya haraka kutokana na hali ya mgonjwa kuwa mbaya.

Amesema licha ya mama huyo kufika akiwa katika hali mbaya alijitahidi kujieleza ili apate huduma kwa waaguzi waliokuwa zamu akiwemo mtuhumiwa huyo Patricia Kisoti ambaye ndiye aliyetakiwa kumhudumia mgonjwa huyo lakini alishindwa kutoa ushirikiano badala yake alitoa majibu ya kejeli na kushindwa msaada wowote.

Amesema kama mama huyo angemshughulikiwa kwa haraka ikiwa na muuguzi huyo kutoa taarifa kwa ngazi za juu baada ya kuona tatizo hilo haliwezi, basi mtoto huyo angekuwa hai.

Aidha, Mkuu huyo alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya, Sophia Kumbuli kuhakikisha anachukua hatua za kinidhamu kwa wahusika wote.Amesem kifo cha kichanga hicho, kwa asilimia kubwa kilitokana na uzembe wa muuguzi huyo kutokana na maalezo yaliyotelewa mgonjwa huyo.

Akizungumzia sakata hilo, Maria Solomoni, amesema siku hiyo, yeye akiwa ameongozana na mwenzake aliyemtambulisha kuwa alikuwa ni wifi yake, walifika katika kituo hicho cha afya majira ya usiku, huku akiwa ameshikwa na uchungu, ambapo waligonga mlango wa chumba cha nesi ambao kwa muda huo ulikuwa umefungwa.

Maria, aliendelea kufafanua kuwa aliendelea kuteseka na mates ohayo mpka majira ya saa kumi namoja alifajili ndipo alipoona wanaume wawili wakimuhangaikia na kumuingiza katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa oparesheni.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya, Sasita Shabani, alikiri kutokea kwa tukio hilo kituoni hapo na kwamba katika uchunguzi wao wa awali umebaini kwamba katika tukio lililomkuta Maria Solomoni, ndani yake kulikuwa na uzembe.

Chanzo: Michuzi