Prof Ndalichako awashangaa Waandishi.



Waziri mwenye dhamana ya  Elimu nchini,  Prof Joyce Ndalichako amesema taarifa ya kwamba Wanafunzi 66,000 wamekosa Mkopo ni ya uongo na ilitolewa bila kujua Takwimu sahihi.

Akihutubia Wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi katika Majengo ya Malazi kwa ajili ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam inayoendelea Muda huu, Prof Ndalichako amesema " Wanafunzi wakiodahiliwa hawazidi 58,000 inawezekana vipi waliokosa Mikopo wawe 66,000? ". Prof Ndalichako amesisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kutoa Mikopo kwa Wanafunzi wengi mwaka huu kuliko mwaka jana.