Sababu ya Bei za Viwanja na Nyumba kushuka kwa kiwango Kikubwa



Suleiman Pazi ni Mkurugenzi wa kampuni ya Makazi Solution Tanzania LTD amezitaja sababu za kushuka kwa bei za viwanja katika miji tofauti, alipokuwa anahojiwa na Redio ya Clouds katika kipindi cha asubuhi.

Kayasema haya kuhusu bei za viwanja na Nyumba

Kwenye sekta ya biashara ya kuuza nyumba na viwanja ( Real Estate) kumekuwa na hali ambayo tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma, sasa hivi bei ya nyumba na viwanja imeonekana kushuka kwa kiwango kikubwa kutokana na hali ya kiuchumi yaani watu waliokuwa walinunua viwanja na nyumba sio wengi kama miaka iliyopita, Suleiman Pazi ni Mkurugenzi wa kampuni ya Makazi Solution Tanzania LTD wanaousika na upangaji miji Mijini na Vijijini anazungumzia sababu ya kushuka kwa bei ya viwanja na nyumba.