SAKATA LA KUPIGWA MWANAFUNZI MBEYA: WABUNGE WAWILI KUBUZURWA KORTINI.

Kufuatia sakata la kupigwa mwanafunzi katika shule ya sekondari Mbeya day, kijana Frank Ludwiko Msigwa anatarajia kuwapandisha kizimbani wabunge wawili, Seif Hamis Gulamali na Elibariki Kingu wote wa CCM kwa madai ya kumchafua mitandaoni (Defamation) kinyume na sheria ya mitandao no.14 ya mwaka 2015 na sheria ya magazeti no.4 ya mwaka 1976.



Katika sakata hilo kijana Frank L. Msigwa ambaye ni kada wa CHADEMA na mwanafunzi wa ualimu chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa, mkoani Iringa, analalamika picha zake kutumiwa vibaya na kufananishwa na kijana mwenye jina kama lake aitwae Frank Msigwa mwanafunzi wa shahada ya ualimu Chuo Kikuu kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).

Frank Msigwa mwalimu wa mazoezi anayedaiwa kumpiga mwanafunzi huko Mbeya ni mwenye picha kulia (B) na Frank Msigwa kada wa Chadema ni mwenye picha kushoto (A).

Wabunge hao wawili wa CCM wanadaiwa kula njama (conspirancy) na kusambaza picha za Frank Msigwa mwanafunzi wa Mkwawa ambaye ni kada wa Chadema wakimhusisha na tukio la kumpiga mwanafunzi huko Mbeya, badala ya Frank Msigwa mwanafunzi wa DUCE ambaye ndiye aliyehusika na tukio hilo.

Wabunge hao walifanya hivyo wakiwa na nia ovu (malice aforethought) kwa lengo la kupotosha ukweli wa tukio hilo na kumchafua kijana huyo kwa sababu tu ni kada wa Chadema. Inadaiwa walifanya hivyo huku wakijua ni kosa kosa kisheria, na walipotakiwa kuomba radhi na kuweka usahihi wa taarifa hiyo hawakufanya hivyo.

Tayari mawakili wa upande wa mashtaka wamekamilisha ushahidi unaoonesha kuwa Frank Msigwa aliyetajwa na wabunge hao wa CCM sio Frank Msigwa aliyempiga mwanafunzi huko Mbeya, hivyo wabunge hao wana kesi ya kujibu.

Malisa GJ