Tyson Fury amesema amekuwa akitumia Cocaine ili kumsaidia kukubiliana na matatizo ya kiakili.

Bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Tyson Fury amesema amekuwa akitumia Cocaine ili kumsaidia kukubiliana na matatizo ya kiakili.



Bondia huyo wa Uingereza amesema kuwa amekuwa akiugua ugonjwa wa kiakili kwa miaka kadhaa na hajafanya mazoezi tangu mwezi Mei.
Nimekuwa nje nikilewa ,Jumatatu hadi Ijumaa hadi Jumapili na kutumia Cocaine,Fury aliambia jarida la Rolling Stones.

Hatua hiyo inajiri siku mbili baada ya Fury kudai katika mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu,kabla kukana madai hayo saa tatu baadaye akisema alikuwa akifanya utani.

Akizungumza kuhusu maswala ya afya yake ,Fury aliongezea: Siwezi kukabiliana na matatizo haya na kitu kinachonisaidia ni wakati ninapokunywa ili nitoe matatizo hayo akilini.wanasema nina ugonjwa wa kiakili.Nahisi huzuni.Niingependa mtu aniue kabla sijajiua.

#BBC