Na. Yericko Nyerere
1.Alizaliwa tarehe 13/04/1922 Butiama na kufariki tarehe kama ya Leo 14/10/1999 kule London.Ni Raisi wa kwanza Afrika kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.
2.Ni Raisi wa kwanza kuhama Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoijenga kwa mkopo akiwa bado Raisi.
3.Ni kati ya Raisi aliyekuwa analipwa mshahara mdogo duniani na pengine kati ya raisi aliyewahi kulipwa mshahara mdogo barani Afrika mpaka sasa.
4. Ni Mtanganyika wa kwanza kusoma chuo kikuu nchini Uingereza na Muafrika wa pili kupata Degree nje ya Afrika, akisomea English, Political Economy, Social Anthropology, British History, Economic History, Constitutional Law, and Moral Philosophy.
5. Ni kiongozi aliyeisaidia China kuingia Umoja wa Mataifa na hotuba yake maarufu akisema
kwamba,"Umoja wa Mataifa si serikali ya dunia bali ni sehemu ambayo dunia nzima inakutana,
kwahiyo kumtoa China katika umoja wa mataifa ni kumtoa kuwa sehemu ya dunia".
kwamba,"Umoja wa Mataifa si serikali ya dunia bali ni sehemu ambayo dunia nzima inakutana,
kwahiyo kumtoa China katika umoja wa mataifa ni kumtoa kuwa sehemu ya dunia".
6. Ndio mwanzilishi wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini- Anti Apartheid Movement mwaka 1959 pamoja na Trevor Huddleston nchini Uingereza.
7. Ni mmoja kati ya waanzilishi wa Umoja wa Afrika, 1963.
8. Amezisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kuliko mtu mwingine yoyote katika historia ya ukoloni, nchi hizo ni Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) and Seychelles (1976) na baadae 1975 (Mozambique), (Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990
(Namibia) na 1994 (South Africa).
(Namibia) na 1994 (South Africa).
9. Mwaka 2009 alitajwa na raisi wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kama "World Hero of Social Justice".
10. Amepokea shahada mbalimbali kutoka, University of Edinburgh (UK), Duquesne University (USA), University of Cairo (Egypt), University of Nigeria (Nigeria), University of Ibadan (Nigeria), University of Liberia (Liberia), University of Toronto (Canada), Howard University (USA), Jawaharlal Nehru University (India), University of Havana (Cuba), National University of Lesotho, University of the Philippines, Fort Hare University (South Africa),Sokoine University of Agriculture (Tanzania), and Lincoln University (PA, USA).
11. Alipokea Tuzo ya Order of José Marti Cuba 1975, Order of the Aztec Eagle (Collar) Mexico 1975, Order of Amílcar Cabral Guinea Bissau 1976, the Nehru Award for International Understanding in 1976, the Third World Prize in 1982, Order of Eduardo Mondlane.
Mozambique 1983, the Nansen Medal for outstanding services to Refugees in 1983, Order of Agostinho Neto Angola 1985, Sir Seretse Khama SADC Medal 1986, Joliot-Curie Medal of Peace 1988, the Lenin Peace Prize in 1987, the International Simón Bolívar Prize in 1992, and the Gandhi Peace Prize in 1995, Statesman of the 20th century by the Chama Cha Mapinduzi 2000, Order of the Companions of O. R. Tambo (Gold) South Africa 2004, Royal Order of Munhumutapa Zimbabwe 2005, Most Excellent Order of the Pearl of Africa (Grand Master) Uganda 2005, Order of Katonga Uganda 2005, National Liberation Medal Rwanda 2009, National Liberation Medal Rwanda 2009, Campaign Against Genocide Medal Rwanda 2009, Order of the Most Ancient Welwitschi Mirabilis Namibia 2010, Tanzania Professional Network Award 2011, Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Tanzania 2011, National Order of the Republic (Grand Cordon) Burundi 2012 and Order of Jamaica, Jamaica.
12. Mwaka 2007 Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimpa tuzo ya Katongo, Medali ya juu kuliko zote ya Jeshi la Uganda kwa heshima ya upinzani wake dhidi ya ukoloni na serikali ya Idi Amin.
13. Mitaa, barabara, majengo, vituo, shule, vyuo na vitu vilivyopewa jina lake; Daraja la Nyerere Kigamboni,Julius Nyerere University of Kankan, in Kankan, Guinea, Nyerere Drive,Gaborone (1.6 km) in Botswana, Nyerere Avenue, Mombasa (1.5 km) and Nyerere Road, Kisumu (2 km) in Kenya, Julius Nyerere Street, Windhoek (1.1 km) in Namibia, Julius Nyerere Street, Durban (0.5 km) in South Africa, Nyerere Road, Kitwe (1.4 km) in Zambia, Julius Nyerere Way, Harare (1 km) in Zimbabwe, Julius Nyerere International Airport, Julius Nyerere International Convention Centre, Nyerere Day- Public Holiday 14/10, Nyerere Cup, Nyerere Road, Unguja, Zanzibar (6.5 km), Nyerere Secondary School in Mwanga District and J.K. Nyerere Secondary School in Moshi, Kilimanjaro Region, Mwalimu J. K. Nyerere Secondary School in Mbozi District, Mbeya Region, Nyerere Memorial School in Korogwe, Tanga Region, Nyerere High School Migoli in Iringa Region, Nyerere Secondary School in Unguja, Zanzibar, Mwalimu Nyerere Foundation, Mwalimu Nyerere Museum Centre and Mwalimu Nyerere Memorial Academy- Tanzania.
14. Baadhi ya vitabu alivyoviandika ni, Freedom and Unity (Uhuru na Umoja), Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa), The Arusha Declaration, Education for self-reliance, The varied paths to socialism, The purpose is man, Socialism and development, Freedom and Development (Uhuru Na Maendeleo), Ujamaa, Crusade for Liberation, Education for Self-Reliance, na Uongozi na Hatima ya Tanzania.
15. Pamoja na kujulikana kama - Baba wa Taifa la Tanzania, Nchi za Kusini mwa Afrika zinamtambua kama baba wa Ukombozi wa Nchi za Kusini.
16. Pamoja na kujua lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa Ufasaha - pia alikuwa akifahamu lugha ya Kigiriki na Kilatini.
17. Julius Nyerere ameandikwa kwenye kitabu cha Enyclopia kama mtu pekee duniani katika historia ya karne ya 21, aliyeweza kuwafanya watu wa makabila, dini, asili na historia tofauti kujiona kama watu wamoja.