BIFU ZA WASANII WA MUZIKI WATANGAZAJI WANACHOCHEA??, ZINA MASLAHI ??

Mahundi E

Karimu Ndugu msomaji wa Mtandao huu wa SocialMedia Habari katika Kipengele cha Uchambuzi kuhusu Muziki na Sanaa ya Tanzania. Leo tutazungumzia kuhusu Muziki wa Tanzania na Kujikita zaidi hasa Katika Bifu za Wasanii, kuchambua kuhusu Watangazaji kuchangia kukua kwa Bifu hizo.Vilevile tutajadili maslahi ya Bifu hizo katika kukua kwa Mziki wetu na Mapato kwa wasanii.



Kabla ya kuangalia Bifu za wasanii katika kipindi ambacho Muziki umekuwa na mchango mkubwa na kukubalika na sehemu kubwa ya jamii na kuamini kuwa, kuwa mwanamuiziki ni jambo jema na ni sehemu ya Ajira. Hebu tupate kufahamu baadhi ya Bifu zilizowahi kutokea katika kipindi cha Nyuma.

Dudubaya na Mr Nice

Mr Nice na Dudu Baya ni wasanii waliofanya Vizuri sana katika kipindi cha Miaka ya Nyuma na Kujizolea umaarufu mkubwa kwa Mashabiki na Album zao kuuzwa zaidi. Hata hivyo wawili hawa waliingia kwenye misuguano na Kupelekea Ugomvi kati yao. Katika Bifu ambalo lilikuwa kubwa sana na mitandao ya kijamii ingekuwa basi lingekuwa kubwa zaidi.

Wawili hawa walionesha kuwa na bifu zito baada ya Dudu Baya kumtwanga makonde Mr Nice mbele ya mashabiki wake na kufikishana mahakamani ambapo Dudu baya aliswekwa rumande. Hata hivyo, wawili hao katikati ya mwaka jana 2015 walimaliza tofauti zao huku picha yao wakiwa pamoja ikizua gumzo kwenye mitandao kibao Bongo.

Tid Vs Q–Chillah

Ni moja ya wasanii wakongwe katika Muziki wa Bongo Fleva na walifanya vizuri miaka ya nyuma na bado wanasikika kwenye kazi tofauti. Ila nao walishawahi kuwa katika mahusiano yasiyo kuwa mazuri.

Wawili hawa waliungana na kutengeneza bendi waliyoiita Top Band na kufanya ngoma kali ya Nilikataa, lakini baadaye wakafarakana na kila mmoja akawa kivyake huku wakirushiana maneno kila mara, mwaka 2015 wakongwe hawa walipatanishwa na kuahidi kufanya kolabo ya pamoja ili kuwaonesha mashabiki wao kama wamepatana.

Bob Junior Vs Diamond


Bifu ya Diamond na Bob Junior siyo ya siku nyingi japo ilivuma sana ukizingatiwa kuwa Bob Junior ndiye aliyemtoa Diamond baada ya kumtengenezea nyimbo nyingi ambazo zilifanya vizuri na kumtambulisha katika Muziki.

Bob Junior ambaye ni prodyuza aliyemtambulisha Diamond kwenye gemu, aliingia bifu na msanii huyo kiasi cha kuacha kufanya kazi pamoja na bifu hilo likikolezwa na vita ya nani Rais wa Sharobaro huku ikidaiwa kuwa na figisufigisu nyingizi mbali na sababu hiyo. Hata hivyo, wawili hawa walionesha kumaliza tofauti zao na katika shoo ya Zari All White Party iliyofanyika Mei mwaka jana ambayo ilimuhusisha mwandani wa Diamond, Bob Junior alijumuika nao na kufurahi pamoja kuonesha kuwa hawana bifu tena.

Nay wa Mitego Vs Madee


Na hii ni moja ya Bifu ya Miaka ya hivi karibuni ambayo ilivuma sana hasa kwa kuwa wote wanatokea maeneo ya Manzese.

Bifu la wakali hawa lilianza kama utani kwa kugombania hadhi ya Rais wa Mazense ambapo kila mmoja alidai kuwa na haki hiyo kiasi cha wawili hao kutajwa kufanyiana fujo hata kwenye shoo. Hata hivyo, walipatana mwaka 2014 na kuwashangaza watu kwa kupeana lifti na kupiga picha wakiwa kwenye gari moja.

Bifu zingine zilizotikisa katika Muziki wa Bongo Fleva Inspector Haroun na Juma Nature, O’Ten vs Afande Sele na nyingine nyingi.

BAADA YA KUANGALIA BIFU AMBAZO ZIMETOKEA KATIKA KIPINDI CHA NYUMA 

NA SASA TUANGALIE BIFU AMBAYO INAZIDI SHIKA KASI SIKU HIZI ZA HIVI KARIBUNI KATI YA ALIKIBA NA DIAMOND


Kipindi cha Nyuma wasanii hawa walikuwa washikaji na Alikiba kipindi hicho yeye alikuwa juu zaidi Kimuziki ukilinganisha na Diamond.

Chanzo cha Bifu lao inasemekana kwamba Kuna Nyimbo ambayo Diamond alimshirikisha Alikiba na baadae kufuta kipande alichoimba Alikiba na Vile vile kuna tetesi kuwa katika Wimbo wa Alikiba wa Single Boy kuna Kipande cha Diamond kilifutwa japo Alikiba alikanusha kuwa Hakuwahi kufanya Nyimbo na Diamond.

Pande zote mbili zinakataan kuwa hakuna Bifu baina yao, Upande wa Alikiba na upande wa Diamond. Japo kwa Mashabiki majibizano na magambo baina ya Mashabiki pande zote mbili ni makubwa hasa katika Mitandao ya Kijamii na mtaani.

Mwaka huu 2016 Alikiba akiwa kwenye Tamasha Kenya ambalo Chrissbrown, Wizkid na Alikiba watumbuiza kulitokea taharuki baada ya Mic kuzimwa katika kati ya Show ya Alikiba. Na kupelekea malalamiko kwa Alikiba kuwa wakati anatumbuiza Meneja wa Diamond alikuwa Backstage na haliusika kwenye tukio, Na Alikiba alipohojiwa alisema "Yeye na Diamond hawapo katika mahusiano mazuri inakuwaje Meneja wa Diamond anakaa Backstage na ikiwa hana msanii wake anayetumbuiza"

Na siku za Hivi karibuni kumekuwa na shutuma kuhusu kununua Views Youtube na Mwingine akijibu kuwa Muziki sio sauti pekee. Kama muziki ni sauti basi Wema Sepetu angechukuliwa kuimba.

NINI SABABU YA BIFU HILI NA KITU GANI KIFANYIKE?? KUNA HAJA YA KUENDELEA KUWA NA TEAM ZA WASANII


Sababu kuwa ya Bifu hii ni kwa kila msanii kujiona ni bora kuliko mwenzake. Alikba anajiona ni bora zaidi katika muziki wake na muziki wake ni mzuri zaidi ya mwenzie na Diamond akijiona bora ya Alikiba na muziki wake ni mzuri na amefika mbali zaidi kimuziki ukilinganisha na Mwenzie.

KUNA HAJA YA KUENDELEA KUWA NA TEAM ZA WASANII??

Kwa maoni yangu kuna haja ya wasanii kuwa na Team kwa sababu hawa ndio Mashabiki na ndio wanaosapoti muziki wake ila Team za wasanii ziwe za Kibiashara na sio Team za Matusi na Kejeli. Karibu sehemu kubwa ya Team za Diamond na Alikiba ni za Matusi na Kejeli hasa katika Mitandao ya Kijamii. Na ili Team hizi ziwe za Kibiashara Msanii husika anawajibu wa Kubadili mwenendo huu na Kuipa Biashara ifanyike na Kujiongezea Kipato.

Vitu hivi Muhimu kufanya Ili Team ziwe na Tija Kibiashara

Mashabiki wa Msanii wawe ndio watu wa Kwanza kununua Kazi za msanii
Mfano kwa Msanii mwenye Mashabiki Milioni Moja na akatoa Nyimbo yake Mashabiki zake wawe watu wa kwanza kununua Kazi hiyo. Mfano Nyimbo Moja Msanii ikauzwa kwa Shilingi 400 na Mashabiki zake laki tano wakanunua Nyimbo hiyo, Msanii ataingiza Kiasi cha shilingi 200,000,000 ( Milioni mia mbili kwa Nyimbo moja). Kupitia ushabiki unamuwezesha msanii wako kwa kiasi kidogo na Msanii akaingiza kiasi kikubwa na pesa na Serikali kupata Kodi. Huu ndio ushabiki wa kisasa na Uteam wenye maslahi kwa msanii wako na sio kutukana mtandaoni.

Na sio kununua Nyimbo pekee bali ndio wawe watu wa kwanza kununua Album za wasanii na Bidhaa zingine za msanii.

Mashabiki wa msanii wawe watu wa kwanza kuhudhuria Kwenye matamasha ya msanii wao

Uteam kama ungekuwa unatumika kuhudhuria kwenye matamasha ya msanii ungesaidia kuboresha vipato vya Wasanii. Mashabiki wa msanii wawe watu wa mwanzo kuhudhuria matamsha ya msanii wao na kufanya matamsha kujaa watu. Mfano mtu mwenye Mashabiki Laki tano na kwenye tamasha lake wakahudhuri watu elfu thelathini (30,000) kwa Kiingili cha elfu kumi (10,000). Msanii ataingiza kiasi cha shilimgi 300,000,000 (milioni mia tatu). Huu ndio uteam wa kisasa katika kiwango cha 4G.

Kuna Vitu vingi Team za Wasanii wanaweza kufanya kwa msanii wao kwa kuleta Tija Kubwa kwa msanii Kimapato na hata Kijamii.

Asante kwa kusoma, Tukutane tena siku nyingine katika Uchambuzi kuhusu wasanii na sanaa kwa Ujumla.

Wako Mtiifu
Emmanuel Mahundi