KIPA MGHANA WA SIMBA ATUA

Dar es Salaam. Kipa Daniel Agyei ametua nchi leo saa saba mchana akitokea nchini Ghana kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba. Agyei aliyekuwa anaichezea Medeama, amewasili kwa ndege ya Shirika la KQ na kupokelewa na mratibu wa timu ya Simba, Abbas Ally.



Baada ya kutua, kipa huyo amepelekwa kwenye hoteli ya Sapphire jijini kabla ya kukutana na uongozi wa Simba kwa ajili ya kusaini mkataba huo. "Kwa sasa anakwenda kupumzika na  leo jioni au kesho ndipo atakutana na viongozi kwa ajili ya kukamilisha usajili wake," anasema Abbas