MABINGWA wa soka Tanzania bara wameendelea kuongoza katika orodha ya vilabu bora kwa Tanzania

MABINGWA wa soka Tanzania bara wameendelea kuongoza katika orodha ya vilabu bora kwa Tanzania kufuatia viwango vilivyotolewa na CAF, katika bara la Afrika Yanga SC ipo nafasi ya 331, Azam nafasi ya 351 huku Simba wakiburuza mkia katika tatu bora nchini wakiwa nafasi ya 356.



Hans Van Pluijm amesema " Yanga SC ni miongoni mwa klabu kubwa na kongwe barani Afrika, kwa umri iliyonayo yapasa kuwa 100 bora ama 50 bora, Lakini nafurahi kuona ndio klabu bora kwa Tanzania inabidi sasa tupigane kuisogeza mahala stahiki"

Iliyokuwa klabu ya kocha mpya wa Yanga , Zesco United ya Zambia inashika nafasi ya 47 huku vilabu vya Tunisia Esperance de Tunis na Etoile du sahel vikishika nafasi ya kwanza na ya pili kisha Tp Mazembe ya tatu.

Kwa kumchukua George Lwandamina kisha Hans Van Pluijm akiwa mkurugenzi wa ufundi, Klabu ya Yanga inategemea kufanya makubwa katika michuano ijayo kutokana na weledi mkubwa wa waalimu hao.