Ndege iliyobeba Wachezaji wa Klabu ya Soka Brazil Yaanguka

Ndege iliyobeba watu 81 wakiwemo wachezaji wa klabu ya soka ya Chapecoense kutoka Brazil imeanguka wakati ikikaribia kutua katika mji wa Medellin nchini Colombia, mamlaka zathibitisha.



Taarifa kutoka eneo la tukio zinaarifu kuwa watu 76 wamefariki dunia huku watano wakipona. Maofisa wa uwanja wa ndege wa Medellin wamesema wachezaji wa Chapecoense waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa safarini kwenda kucheza fainali ya Copa Sudemericana dhidi ya Atletico Nacional ya Medellin, Colombia.

Kutokana na ajali hiyo, mechi baina ya timu hizo iliyokuwa ichezwe kesho imeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.