Ney wa Mitego asema hajambaka Nisha Bebee, Naye Nisha Atoa ya Rohoni

Ney wa Mitego na Nisha waliwahi kuwa wapenzi miaka na Uhusiano wao ukavunjika. Siku za Hivi karibuni Nisha amekuwa akitoa shutuma kwa mwanaume ambaye amempatia ujauzito na bila kutaja jina la mwanaume huyo. Baadhi ya Mashabiki katika Mitandao na Magazeti wamekuwa wakimuhusiha Ney wa Mitego katika Kashfa hiyo.

Ney  na Nisha Bebee


Naye Ney akajibu shutuma hizo dhidi yake na Kusema kuwa ana miaka zaidi ya miwili hajwahi kuwa karibu na Nisha na hata hajawahi kuonana nae.

Ujumbe alioandika Ney Hua sipendi Marumbano na watoto wa Kike kabisaaa.! Hata ikitokea akanichafua mi hua nakaa kimya coz naamini Mwanaume ukijibishana na Mwanamke utakua hujielewi na watu watakudhalau. Mi hua nasubiri majibu itajulikana nani mkorofi.

But kwa hili la #Nishabebe naona linaenda pabaya Acha niongee kidogo....
Ni hivii... Nina Mwaka wa pili 2 Kama Sio watatu 3, Sijamtia machoni huyu dada, yaani hatuja onana face to face kwa kipindi icho. Cha ajabu naona magazeti yana andika, na Mitandao (PageZaUmbea) Eti nime Mbaka huyu Mcheza Sinema za bongo. Maninaaaaa cjashindwa wanawake kiasi Cha kumbaka huyo Bibi kizee wa Masinema leee.😡😡. Nisha tafadhari heshima hainunuliwi ata cku 1 usipo omba Radhi kwa hili utakua na kesi kwangu. Kama ni kick Sio kwa style ya kunichafua eti nimekubaka na una mimba😡😡.! Please nasema Hivi narudia tena, cjaonana na huyu Bibi zaidi ya miaka miwili. Sitaki kusikia Huu ujinga tena.. Nina Mwanamke mzuriiiii akivua tu Nguo la kwanza, nikimsogelea mapajani la pili, alafu msafii..! Nika mbake uyo Bibi wanini..?! Tafadhari izo kick zako zitakuja kukutokea puani.! Sijui ndo unataka uuze izo parfume zako....?! Tafuta gear nyingine.! SipendiUjinga.!

Baada ya Ney kujibu shutuma zinazosambaa dhidi yake katika mitandao naye Nisha Bebee aka,jibu Ney kupitia Instagram na Kusema #Naywamitego  iko hivi kabla hujaandika kitu chunguza sio unakurupuka tu na kuandika ujinga.
ulinisikia na kuniona wapi nimekutaja kwamba wewe ndo baby dady wangu???? hivi naanzaje kuzaa na wewe Nay?? kifupi pamoja na mapungufu na makosa yaliyojitokeza kwa baba k wangu humfikii hata kwa kucha labda umemshinda hizo tatoo zako kama bibi harusi.
Nikuombe msamaha kwa kipi acha kudandia treni kwa mbele.??? tena watishe hao hao WANAUME SURUALI mimi simuogopi yeyote anayekojoa akiwa amesimama wala amechutama.
tena USINICHOKONOE
nb:chanzo chako cha kutagiwa labda nikufunue akili yako ni hiyo coment huyo ni mimi???? nna mahusiano naye??.. next time tumia akili.
#NASEMA# HIVIIIII #SIMUOGOPI #MTU YETOTE