NISHA BEBEE ATOA CHOZI, AKOSA AMANI YA MOYO

Nisha Bebee toka apate Ujauzito kwa Mwanaume ambaye hakuwa tayari kuzaa naye. Amekuwa katika hali ambayo sio nzuri, ni pale alipoamua kuandika ujumbe kuhusu mwanaume ambaye amempatia Mimba hiyo bila kumtaja Jina. Na alisema mwanaume huyo aliwahi kuwa na mahusiano naye kipindi cha Nyuma.

Nisha Bebee


Na walisha achana na alikuwa na mapenzi na mtu mwingine, na kwamba alimuingilia bila yeye kuwa tayari. Ni kwa sababu tu anajua uzaifu wake.

Leo katika akaunti yake ya Instagram amepost Video akiwa analia na kusema kuwa bado ana hamani ya moyo kabisa katika kipindi hiki. Na kuandika haya  UNAJUA KINACHOUA UZURI WNG?? NI MACHOZI YANITOKAYO KILA SIKU. Naweza kwenda popote,naweza nunua chchte nnachotaka.. M'Mungu kanibariki neema zote kubwa na ndogo.. kitu pekee ambacho sina ni AMANI YA MOYO WANGU