SERIKALI YAOKOA BILION 1.3 KWA UNUNUZI WA MAGARI YA UMMA

SERIKALI kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), imeokoa Sh bilioni 1.3 baada ya wakala huyo kununua kwa pamoja magari 392 katika mpango wa serikali wa manunuzi ya pamoja.



Kaimu Mtendaji Mkuu wa GPSA, Jacob Kibona alisema jana kuwa, fedha hizo zimeokolewa na serikali baada ya kununua magari 392 kwa pamoja kwa Sh bilioni 56.1 badala ya Sh bilioni 58.1 iwapo kila taasisi ingenunua magari yake.
“Kwa kweli huu mpango wa manunuzi ya pamoja ni mpango mzuri sana ambao unaiwezesha serikali kuokoa fedha nyingi,” alisema Kibona na kuongeza kuwa fedha zilizookolewa zitaiwezesha serikali kufanya shughuli nyingine za maendeleo ya umma na kama vile kuboresha miundombinu ya barabara, huduma za afya na elimu.

Aliongeza kuwa, taasisi yake pia katika kipindi cha Julai hadi Oktoba mwaka huu, imezikabidhi taasisi za serikali magari ya aina mbalimbali yapatayo 136