SONGEA: Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea nusura wapigane



Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea nusura wapigane jana baada ya Meya kukataa kuulizwa maswali ya papo kwa papo.

Mzozo huo umekuja baada ya Meya kudai kuwa utaratibu wa kuuliza maswali hayo haukufuatwa hali iliyofanya diwani Ndomba kutolewa nje na kusema Diwani atakayemgusa wataumizana.