WOSIA WA SITTA KWA JK KUHUSU MAGUFULI

Saa chache kabla ya kusafiri kwenda Nchini Ujerumani  kutibiwa marehemu Sitta alliacha ujumbe mzito kuhusiana na mwenendo wa Serikali ya Rais John Magufuli kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.Taarifa  zandani za familia zinasema Sitta aliacha ujumbe mzito kwa Mh  Kikwete kuwa  “Kwa sasa  Rais Magufuli asiachwe kwenda aendavyo kwasababu katika uongozi wake  yapo mambo yanayoenda  sawa na yasiyoenda sawa”



Marehemu Sitta aliacha Ujumbe huo kwa  Rais Mstaafu  Jakaya Kikwete ambae alikwenda kumjulia hali nyumbani kwake masaki Dar es salaam tarehe 31 oktoba  saa chache kabla ya kuondoka kwenda  nchini Ujerumani kwa matibabu ya tezi dume.

Rais mstaafu Kikwete ambaye anatajwa kuwa  alikuwa na mahusiano ya karibu na marehemu  Sitta ailikwenda kwa Marehemu Sitta kumnasihi na kumuondosha hofu  katika matibabu kwani hata yeye  alikumbwa na ugonjwa huo na alifanikiwa kupona  baada ya kufanyiwa uparesheni nchini Marekani.
  
Mmoja wa wanandugu wa Marehemu Sitta ambae alikuwepo siku Mh Kikwete alipomtembelea Marehemu Sitta alisema wawili hao walifanya mazungumzo marefu kwa zaidi ya masaa matatu ambapo  marehemu Siita alionesha kwamba alikua na jambo zito alilotaka kumueleza Mh kikwete  kabla ya safari ya  kwenda Ujerumani kwa matibabu.

“Marehemu alimweleza Kikwete kuwa yeye na wastaafu wenzake wasimuache Rais Magufuli peke yake wampe ushauri hasa kwenye maswala ya uchumi” alisema mwanandugu huyo.

Katika mazungumzo ya marehemu Sitta alimtaka Kikwete atoe ushauri kuhusu mwenendo wa uchumi usivyo ridhisha na manung’uniko ya wananchi kuwa hali ya maisha inazidi kuwa ngumu.

Aliongeza kuwa  baada ya Kikwete  kuona kuwa mzee Sitta alikuwa akizungumza bila kujali muda wake wa kuwasili uwanja wa ndege alilazimika kumkatisha mara kwa mara kumtaka aondoke kwa hofu kwamba angechelewa ndege.

Marehemu hakuonesha kujali kuchelewa kwake na kuzidi kumsisitiza kuwa  afanyie kazi maagizo yake ya kumshauri  Rais kwenye baadhi ya maeneo muhimu kwa mustakabali wa nchi na Chama Cha Mapinduzi.

Chanzo: Fahari News