BARUA INAYODAIWA NI YA GODBLESS LEMA ALIYOANDIKA AKIWA RUMANDE KWENDA KWA JOHN MALYA

Jana mmoja wa wanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Malya alifunga ndoa ambapo viongozi mbalimbali wa chama hicho walijumuika pamoja naye.

 Godbless Lema


Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema hakuweza kuhudhuria sherehe hizo sababu yupo rumande kutokana na kesi ya uchochezi inayomkabili. Aidha, kuna barua hii ambayo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikielezwa kuwa inatoka kwa mbunge huyo kwenda kwa John Malya.

Kikubwa kinachoelezwa katika barua hii inayodaiwa ni ya mbunge huyo ni nia yake kubwa aliyokuwa nayo kuhudhuria sherehe hiyo ya rafiki yake. Lema amemtakia John baraka kwenye ndoa yake huku akinukuu mistari kwenye biblia usemao “Apataye mke amepata kilicho chema.”

John Malya