IRINGA: Azikwa kaburi moja na Kondoo

MAMIA ya wakazi wa kijiji cha Mbigili na mji wa Ilula katika wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa jana walifurika katika mazishi ya aina yake yaliyofanyika katika kitongoji cha Mkawaganga kijiji cha Mbigili wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kushuhudia mazishi ya kihistoria baada ya mzee mmoja aliyefariki dunia ghafla kuzikwa kaburi moja na kondoo pamoja na kuku mweusi.



Tukio hilo limetokea wakati wa mazishi ya mzee Andrea Ngaga (90) mkazi wa kitongoji cha Mkawaganga aliyekuwa akijishughulisha na kazi za uganga wa kienyeji kijijini hapo enzi za uhai wake .

Baadhi ya wananchi waliofika katika mazishi hayo walisema kuwa walilazimika kusitisha shughuli zao za shamba na biashara na kufika kushuhudia mazishi hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika katika kijiji hicho alisema John Mfaligoha kuwa kabla ya kifo marehemu huyo alipata kuwaeleza aina ya mazishi yake yatakavyokuwa .

Hivyo alisema wananchi waliowengi walifika kutaka kushuhudia tukio hilo la mazishi na ndio sababu iliyopelekea wananchi kusukumana msibani wakati wa mazishi kwa kila mmoja kutaka kushuhudia tukio hilo la kihistoria katika kijiji hicho.