Darassa ashauriwa na daktari kutofanya shoo kwa muda baada ya kupata ajali

Darassa ambaye anafanya vizuri na Nyimbo yake ya "Muziki" Wiki alipata ajali ya Gari na kupelekwa Hospitali. Akiwa anahojiwa Jana katika kipindi cha XXL cha CLOUDS aliyasema haya kuhusu afya yake.

Darassa


"Nipo hospitalini Muhimbili sasa hivi nawashukuru sana madaktari wa hapa wamenipokea vizuri wamenipa huduma nzuri sana, wamenicheki kwa sababu nilikuwa najisikia vibaya sana sehemu za kichwani nashukuru Mungu majibu yanaonyesha kila kitu kipo poa kabisa kuna damage ndogo wanaifanyia kazi naendelea na matibabu ila nimeshauriwa kupunguza mizunguko kwa wiki moja ili niweze kupumzika na kutibu hayo maumivu ya kichwa" @darassacmg #XXL