MTOTO WA MIAKA 14 AFUNGISHWA NDOA MKOANI MOROGORO

Serikali wilayani Malinyi mkoani Morogoro imeliagiza jeshi la polisi kumtafuta na kumfikisha mahakamani kijana aliyeatambulika kwa jina moja asemba kwa tuhuma za kumficha binti wa miaka 14 mhitimu wa darasa la saba mwaka huu baada ya wazazi wake kumuozesha na kupokea mahari yenye thamani ya ng'ombe 30.



Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Malinyi Majura Kasika wakati akifunga mafunzo ya askari 140 wa jeshi la akiba ambapo amesema serikali haitafumbia macho ukatili unaoendelea kufanyika kwa watoto wa kike na na kuwapotezea fursa ya elimu kwa tamaa ya mahari kabla ya wakati wake huku akiwasisitiza askari hao kuwa wa ulinzi wa pembe za ndovu na nyara za serikali kutokana na maeneo hayo kuwa karibu na mbuga ya seruhu.

Kwa upande wao wanamgambo hao wameiomba serikali iwasaidie ajira za ulinzi katika majeshi mbalimbali ya hapa nchini na kampuni binafsi ya ulinzi.