Jela miaka 30 kwa kubaka mtoto wa miaka tisa

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Shabani Huseni(29) baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mtoto wa miaka tisa.



Husein amehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi, Catherine Kihoja baada ya upande wa washitaka kufunga ushahidi wao.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Catherine alisema upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi watano ambao wameweza kuthibitisha shitaka hilo pasina kuacha shaka yoyote. "Kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa umeweza kunithibitishia shitaka hivyo mshtakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshitakiwa,’’alisema Hakimu. #Mwananchi