MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAZIDI KUONGEZEKA



Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba Mwaka 2016, umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.5 mwezi Oktoba, 2016.



Ongezeko hilo linamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2016 imeongezeka ikilinganisha na kasi ya upandaji ilivyokua kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2016.

Mfumuko wa Bei ya Vyakula kwa Mwezi Novemba 2016 umeongezeka hadi asilimi 6.4 kutoka asilimia 6.0 mwezi Oktoba 2016, na kwamba baadhi ya Bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na Mbogamboga kwa salimia (7.1.), Unga wa Mahidi(1.5%), Unga wa Ngano(2.4%), Unga wa Muhogo(1.7%), mtama (1.5%), dagaa wakavu(1.1%) pamoja na mchele (1.0%).