Mke wa Rais Baada ya kuuugua ahudhuria Misa akiwa na Mke wa Majaliwa

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli jana Jumapili aliungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitali.



Akiwa mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wamesali ibada ya asubuhi katika kanisa hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.

Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na wamemuombea afya njema.