SIMBA ‘B’ KUTINGA FAINALI LIGI YA (U20)

Timu ya vijana ya simba ‘B’ imefanikiwa kutinga fainali katika michuano ya vilabu vinavyoshiriki ligi kuu chini ya miaka 20 baada ya kupiga Stand United mikwaju ya penati 8-7 katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 120 ambao ulimalizika kwa suluhu ya bao 1-1 katika, dakika 90 za kwanza, Simba walianza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao Ally Abdallah dakika ya 23 goli lililodumu mpka mapumziko.



Kipindi cha pili Stand United walisawazisha goli hilo kupitia mkwaju wa penati baada ya mchezaji wao kuchezewa vibaya ndani ya boksi la Simba. Matokeo hayo ya 1-1 yalidumu mpaka dakika 90 za mchezo na kuongezewa dakika 30 nyingine ambapo hakuna timu iliyoweza kuongeza goli

Baada ya kumalizika kwa dakika 30 za niongeza timu hizo zilikwenda kwenye hatua ya penati ambapo Simba waliibuka na ushindi wa jumla ya goli 8-7 kwa mikwaju ya penati

Matokeo hayo kwa Simba yanawasogeza kucheza fainali siku ya jumapili tarehe 11/12 mwaka huu na mshindi atakae patikana kwenye mchezo wa Azam dhidi ya ya Mtibwa Sugar unaochezwa leo usiku.