UHUSIANO WETU NA MALAWI NI SHWARI



Serikali ya imesema mzozo kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa kwa sasa unashughulikiwa na jopo la marais wastaafu, na kwamba uhusiano kati ya nchi hizi mbili umeimarika.



Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia taarifa, imesema kwamba licha ya kuwepo kwa mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa, uhusiano wa nchi hizo mbili ni mzuri. "Ukweli ni kuwa, mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwa sasa upo chini ya Jopo la Viongozi Wastaafu wa Afrika wanaotokea kwenye nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)," taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema. "Jopo hilo linaongozwa na Joachim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji akisaidiwa na Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana na Thabo Mbeki, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini." Taarifa hiyo ya serikali imetolewa baada ya wasiwasi kutanda kuhusu uwezekano wa kuzuka tena kwa mzozo kati ya nchi hizi kutokana na ramani iliyodaiwa kutolewa na Tanzania ikionyesha kuwa inaamiliki nusu ya Ziwa Malawi au Nyasa

#BBC