WATU 12 WASHIKILIWA MKOANI KIGOMA KUFUATIA UWIZI WA MIL 11 KWENYE MABENKI

Watu 12 mkoani Kigoma wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kukutwa na kadi 100 za mashine za kutolea fedha(ATM) za mabenki tofauti tofauti.



Watu hao walikuwa wamekwishafanikiwa kutoa fedha katika mashine za kutolea fedha(ATM) kiasi cha shilingi milioni 11.

Kufuatia tukio hilo Kesho la Polisi limewatahadharisha wananchi kuwa makini na wahalifu na matapeli na kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.