Alichopanga kufanya Chege, kitu ambacho ni tofauti na Wenzake

Chege amefunguka na kusema Kwanini bado hana Logo yake na kusema kuwa ukitaka kufanya biashara nzuri ni lazima uwe mbunifu, hivyo yeye amejipanga kufanya kitu ambacho ni cha kitofauti kabisa ambacho watu wengine hawajawahi kukifanya. Unataka kukijua ni kitu gani hicho .

Chege👉“Mimi nitafanya kitu akili yangu inanituma, naweza nisitoe Kofia, nisitoe T-Shirt wala Jeans nikatoa Braslate ya mkononi imeandikwa Chege au kitu kingine, kwanini nitoe kitu ambacho mtu mwingine anacho? Hiyo sio biashara nzuri. Naweza kufanya ila sio T-Shirt wala Kofia wala kitu kingine chochote ambacho watu wameshafanya.” Alisema