MKE MDOGO AJIUA, MUME AKIWA KWA MKE MKUBWA

Mkazi wa kijiji cha Miyogoni kataya Mbugani manispaa ya Tabora, Mwajuma Hamadi , amejinyonga usiku wa kuamkia jana huku sababu za kujinyongakwake zikiwa hazijulikani.

Mtoto wa mwanamke huyo, Tatu Juma, alieleza kuwa walienda kulala na mama yao wakati wa usiku mdogo wake alitaka ampeleke mgodo wake kujisaidia na ndipo walipoanza kumuita mama yake pasipo kuitikiwa.

Mume wa marehemu, Juma Kiligito, alieleza kuwa akiwa amelala na mke mkubwa ndipo majira ya asubuhi, alipoamshwa na mtoto wake aliyemwelekeza kuwa mama yake amejinyonga. Kiligito alisema kuwa hapakuwa na ugomvi wowote kati yake na mkewe huyo a alisema usiku walikuwa wote hadi saa tano wanaangalia runinga.

Mke mkubwa wa Kiligito, Asha naye alisema hawakuwa na tatizo na marehemu a kwamba walikuwa wakiangalia runinga wote na baadae kila mmoja kwenda kulala yeye akiwa na mumewe.

Hata hivyo mama mzazi wa marehemu, Sada Said alielezakuwa siku moja kabla ya kifo chake, mtoto wake (marehemu) alienda kumlalamikia mumewe kuwa hataki ajishughulishe ilia pate kipato. 

Alisema mumewe alimfuata majira yasaa 10 jioni akimweleza kuwa mumewe hataki ashone wakati hali ya maisha ni ngumu kwa vile alikuwa na watoto na wana mahitaji mengi ya kifamilia yanayohitaji fedha. Alieleza kuwa walimsihi arudi nyumbani kwake na yeye(mama) na kaka wa marehemu, wangeenda kuwakutanisha na mumewe na kujua kwa nini haaki ajishughulishe na kushona. Polisi Mokoa wa Tabora Hamis Issa alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa polisi inaendelea na uchunguzi.
#Habarileo -