KAIMU JAJI MKUU AAHIDI MATUMIZI YA TEHAMA

Baada kuapishwa jana na Rais John Magufuli,  Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amesema ataweka mkazo wa matumizi ya mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ili kuhakikisha haki inapatikana kwa haraka kuliko ilivyo sasa.

Kaimu Jaji Mkuu amechukua nafasi ya Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Kabla ya kuteuliwa, Profesa Juma alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa na atakaimu nafasi hiyo hadi Rais Magufuli atakapo fanya uteuzi wa Jaji Mkuu. “Nashukuru Mungu kwa kufika hapa.

Pili Rais (Magufuli) kwa kuniteua, nafahamu kuna wanasheria wengi na vigezo vyote lakini akaniona nafaa,” amesema Profesa Juma mara baada ya kuapishwa.

#Mwananchi