MUUAJI WA WATU 39 ISTANBUL AKAMATWA

Vyombo vya habari nchini Uturuki vimesema mshukiwa mkuu katika shambulizi la mkesha wa mwaka mpya mjini Istanbul amekamatwa. Abdulkadir Masharipov anaaminika kufanya shambulizi hilo ambalo lilisababisha vifo vya watu 39 kwenye klabu ya usiku ya Reina.

#BBC