NAIBU WAZIRI WA AFYA JINSIA NA WATOTO HAMIS KIGWANGALLA AMUANDIKIA UJUMBE HUU RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE

Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Mh. Kigwangala ameandika haya akimkumbuka Rais Mstaafu Kikwete 👇👇👇 Mzee wangu, JK, naendelea kujifunza kitu toka kwako. Hakika wewe ni Mwalimu wangu na Mshauri wangu yakini, unazidi kunifundisha kitu ukiwa mapumzikoni kijijini kwako #Msoga.

Na mimi nimeanzisha shamba langu kijijini Puge. Heri ya Mwaka Mpya kwako, Mkeo na familia nzima. Nikiliona jina #Kikwete, nakumbuka wema ulionitendea na funzo kubwa ninalolipata kutokana na maisha yako kama Kiongozi mashuhuri wa Taifa letu.

Najua wengi wanajifunza. Mbali na mafunzo ninayopata kwako sintosahau ulivyonipa heshima ya kuniteua kugombea Ubunge mara ya kwanza mwaka 2010 japokuwa sikuongoza kwenye kura za maoni. Ulifungua milango yangu kwenye #siasa, ukanilea, ukanilinda, ukanitetea, ukanisimamia siku zote. Maana haikuwa uamuzi rahisi.

Na miaka yangu mitano ya Ubunge ilikuwa ya machozi, jasho na damu. Mara kadhaa nilikamatwa nikipigana vita vya ukombozi wa watu wangu, nikawekwa lock-up, ulipiga simu usiku wa manane nikatolewa! Hakika wewe ni #mzazi kwangu. Kwa wengine ni #Rais Mstaafu, kwangu mimi ni #Baba wa siasa zangu! Ninapotoka kisiasa pagumu sana kuliko nilipofika. Nilipigwa vita, ulisimama na mimi, siku zote. Uliuelewa msimamo na mtazamo wangu. Uliujua ukweli wangu, na uliuvumilia #ujana wangu! Ninapotafakari siasa zangu, malengo yangu ya mwaka 2017 na ya mbele zaidi, baada ya mapumziko kijijini Nzega, nimekumbuka nilipotoka, nikasema nikushukuru publicly leo. Ahsante sana #mjomba wangu!