WAZIRI MKUU AINGILIA KATI UPOTEVU WA KOROSHO

Ruvuma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji awakamate maofisa wanne na kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma za upotevu wa tani 2, 138 za korosho.

Maafisa hao ni Kaimu Meneja Mkuu Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi (Mamcu), Kelvin Rajab na Meneja Tawi wa Mamcu, Lawrence Njozi. Wengine ni wakurugenzi wa kampuni ya YURAP ya Masasi inayohusika na uhifadhi wa mazao kwenye maghala, Yusuph Namkukula na Ramadhani Namakweto.