CANADA KUHALALISHA MATUMIZI YA BANGI MWAKANI

CANADA KUHALALISHA MATUMIZI YA BANGI MWAKANI

Serikali ya Canada imepanga kuwasilisha mswada wa kuhalilisha Matumizi ya Bangi kwa kujiburudisha ifikapo mwaka 2018

Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la nchi hiyo ifikapo Mwezi April mwaka huu kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Serikali nchini humo CBC.

CBC imesema kuwa sheria hizo mpya zitaambatana na mapendekezo yaliyotolewa na jopo lililoteuliwa na serikali.

Baadhi ya mapendekezo hayo ni kuwa  Canada itaruhusu kuuzwa kwa bangi wa kujiburudisha kwa watu walio na zaidi ya umri wa zaidi ya miaka 18 na pia serikali ndiyo itakayo simamia usambazwaji wa bangi hiyo na kuwapa leseni maalum wazalishaji wa Bangi

CHANZO: BBC