JB ADAI YANGA HAIWEZI KUWA YA KIMATAIFA

Msanii Steven Jacob maarufu kama JB amefunguka na kusema klabu ya Yanga ni chanzo cha watu wengi kupatwa na matatizo ya moyo sababu klabu hiyo haina furaha wala haiwapi furaha mashabiki zake ukifananisha na klabu ya Simba. . .

JB amefunguka na kusema toka ameifahamu Simba akiwa mtoto mdogo imekuwa ni klabu ambayo inampa furaha muda mwingi. Amesema timu ya Yanga haiwezi kuwa ya kimataifa kutokana na historia yake ya michezo inayoonesha kutolewa katika baadhi ya mashindano ya kimataifa mara kwa mara. . . .

"Watani zetu wa jadi wanaongoza kwa kuua watu maana wanafungwa kila mara ila mimi binafsi huwa nafurahi sana nikiona wanafungwa na hata kama nikiwa kwenye hasira zangu, mke wangu akija akinionesha video zinaonesha wanavyofungwa huwa 'automatical' nacheka".