ONDOA UOGA KUONGEA MBELE ZA WATU WENGI

ONDOA UOGA WA KUONGEA MBELE ZA WATU WENGI KWA NJIA HIZI KUMI (10)!

1.Wahusishe unaozungumza nao kwa kuwafanya wachangie mjadala kwa kiasi Fulani, ukishajiona uko sawa, anza kutiririka ulichokiandaa sasa.

2.Epuka Kukariri kile utakachokiongea, maana ukisahau kimojawapo, utakwama na hutaweza kuuteka umati wako tena.

3.Kabla ya Kuanza kuongea, ongea na watu kadhaa walioko viti vya mbele maneno mawili matatu ili kulainisha kinywa chako ndipo uanze kuongea.

4.Kipindi kigumu zaidi ni dakika moja kabla ya kuanza kuzungumza mbele ya watu, litambue hili na ukiweza kushinda hapa, umefaulu

5. Vaa mavazi yanayokufanya ujihisi huru siku zote na uliyoyazoea mwilini, Epuka kuvaa nguo yako mpya kwani hili pia linaweza kukufanya ujione mgeni na mwili wako pia.

6.Minya taratibu Misuli ya kinywa (nyuma ya kidevu) kwa dakika kadhaa kabla ya kuanza kuongea

7.Tambua Kuwa, Watu wanaokuangalia hawajui kama huna uzoefu, na hawajali utakapokosea kidogo!

8.Vuta hewa ya Kutosha na kuitoa nje na ongea ukihusisha lugha za mwili

9.Anza na maneno machache yatakayowafanya wacheke.

10.ongea kwa kuvuta irabi (a e i o u) Mfano hawaaaa (badala ya hawa) waleeee (badala ya wale) naniiiiiii (badala ya nani) I said Nooooo (badala ya I said no) nk!