MABASI YA MWENDOKASI YAPATA AJALI

MABASI YA MWENDOKASI YAPATA AJALI
Mabasi mawili ya mwendokasi yamegongana leo asubuhi katika makutano ya Barabara ya Msimbazi na Morogoro jijini Dar es Salaam .

Katika ajali hiyo hakuna majeruhi wala mauti yaliyoripotiwa kutokea na inasemekana watu wote wametoka salama isipokuwa uharibifu wa taa zakuongozea magari katika eneo hilo na uharibifu mkubwa kwa mabasi yenyewe .

Aidha chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana bado hadi pale mamlaka husika itakapotoa taarifa kuhusu ajali hiyo .