UWANJA WA NDEGE WAPEWA JINA LA RONALDO

UWANJA WA NDEGE WAPEWA JINA LA RONALDO

Nyota Cristiano Ronaldo amejipatia heshima nyingine katika kisiwa alichozaliwa Madeira baada ya uwanja wa ndege wa Kisiwa hicho kuitwa jina baada ya lile la mwanzo la Madeira

Ronaldo amepata Heshima hiyo baada ya kuiongoza timu yake ya Taifa kucheza kwa mara ya kwanza kwenye visiwani humo mchezo wa  kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Sweden

Matokeo ya Mchezo huo hayakuwa mazuri kwa Ureno na Ronaldo licha ya heshima hiyo kwakua walifungwa goli 3 dhidi ya 2

Ikumbukwe kuwa Hii sio mara ya kwanza kwa Ronaldo kupewa heshima ndani ya ureno, miaka kadhaa iliyopita mji mkuu wa visiwa hivyo Funchal ulifungua makumbusho maalumu ya Ronaldo pamoja na sanamu kubwa ya Naodha huyo wa Ureno mwenye miaka 31 sasa

Je Unadhani kuna Mmchezaji wa Tanzania anaweza kupewa Heshima hii….?