Waziri Mwakyembe Kuwakutanisha Alikiba na Diamondplatnum

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema ana mpango wa kuwakutanisha pamoja @officialalikiba na @diamondplatnumz mjini Dodoma ili kuzungumza na kujaribu kumaliza kile kinachoelezwa kuwa na ugomvi baina yao.

Wasanii hawa wawili waliteuliwa kwenye kamati ya kuisaidia timu ya taifa ya umri chini ya miaka 17 #SerengetiBoys kufanikisha timu hiyo kufanya vizuri kwenye mashindano ya AFCON yatakayofanyika Gabon mwaka huu. #HabariLeo