NAPE: NITAENDELEA KUWA MTIIFU KWA RAIS MAGUFULI

NAPE: NITAENDELEA KUWA MTIIFU KWA RAIS MAGUFULI

Aliyekuwa Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa, na Michezo Nape Moses Mnauye amesema kuwa ataendelea kuwa mtiifu kwa Rais John Pombe Magufuli,Serikali na Chama cha Mapinduzi tofauti na maneno yanayosemwa mitandaoni

Nape amesema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akimkabithi ofisi Waziri mpya wa wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa, na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe

Tangu Nape alipoachwa kwenye baraza la mawaziri kumekuwa na taarifa nyingi feki kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuenguliwa kwake zikidaiwa kutolewa na Mbunge huyo wa Mtana ambazo hata hivyo amekuwa akizikanusha

“Heshima akiyonipa Rais ni kubwa mno na nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta nchini na nitaendelea kutoa ushirikiano kwa wizara hii kwa sababu mimi ni mdau mkubwa wa sekta hiyo”