NIKKI MBISHI AWAGEUKIA BASATA NI BAADA YA KUONA WIMBO WA NAY UMERUHUSIWA KUCHEZWA

Ni miezi michache sasa imepita toka tusikie wimbo wa I’ m Sorry JK umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kile alichosema Nikki Mbishi kuwa aliambiwa hauko kwenye maadili ingawa Baraza la Sanaa lenyewe halikuthibitisha kuufungia wimbo huo lakini walichothibitisha ni kumuita Nikki Mbishi na kuongea nae. . .

Kupitia akaunti yake ya twitter baada ya kusikia kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Waziri wa Habari,sanaa,utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuruhusu wimbo wa Nay wa Mitego uendelee kuchezwa na pia kuusifia kuwa mzuri,msanii huyo ameuliza vipi kuhusu wimbo wake wa I’ m Sorry JK.

Vipi kuhusu “I’m Sorry JK” ? Ina maana ina maneno makali au mabaya yasiyosikilizika au niaje? alitweet @nikkimbishi