KANISA KATOLIKI LA MBINGA LIMEMFIKISHA MAHAKAMANI MTAWA

KANISA Katoliki Jimbo la Mbinga mkoani Ruvuma, limemfikisha mahakamani mtawa wa kanisa hilo, Emmanuela Nindi (40) kwa tuhuma ya kuliibia Sh milioni 28.8.

Mtawa huyo ambaye alikuwa ni Mhasibu wa jimbo hilo, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya hiyo ili ajibu tuhuma hiyo inayomkabili mbele yake. Ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Seif Kilugwe mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbinga, Magdalena Ntandu kwamba mshtakiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo katika kipindi cha mwaka jana.