MSHAURI WA MANDELA AFARIKI

MSHAURI WA MANDELA AFARIKI
Mwanaharakati za ukombozi wa Afrika Kusini, Ahmed Kathrada aliyefungwa gereza moja na Nelson Mandela, amefariki jana akiwa na miaka 87.

Kathrada aliyefungwa katika gereza la Robben Island hakuingia tena katika siasa mara baada ya kutoka jela na badala yake alichagua kuwa mshauri wa Mandela wakati alipokuwa Rais wa Afrika Kusini.

Mara baada ya Mandela kustaafu na kuachia madaraka baada ya kutumikia kwa miaka minne, Kathrada naye alistaafu na akaanzisha taasisi yake ya Kathrada Foundation.