MAALIM SEIF AVULIWA UKATIBU MKUU CUF

MAALIM SEIF AVULIWA UKATIBU MKUU CUF

Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) Jumanne hii limemvua, Maalim Seif nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Chama hicho na nafasi hiyo kukaimiwa Magdalena Sakaya.

Maamuzi hayo ya Baraza kuu la CUF yametangazwa na Mwenyekiti wa Chama Hicho Taifa Prof. Ibrahim Lipumba alipokuwa  akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam

Pia Prof. Lipumba amesema kuwa Maalim Seif amevuliwa wadhifa huo kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo la kutokufika ofisini bila ya kuwa na taarifa maalum kwa uongozi  wa chama hicho na kutokuhudhulia vikao vya chama

Mbali na hayo, Prof.Lipumba amemtangaza rasmi Abdul Kambaya kuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa Chama hicho.