BASHE : KUNA KIKOSI MAALUM KINACHOENDESHA UTEKAJI NDANI YA USALAMA WA TAIFA


Mbunge wa jimbo la Mnzega Mjini Mh.Hussein Bashe amesema kuwa kuna kikundi maalumu cha utekaji kilicho ndani ya Idara ya usalama wa Taifa na ndicho kinachohusika na utekaji wa watu mbalimbali hapa nchini

Bashe amesema hayo kwenye kikao cha Bunge kinanchioendela mjini Dodoma na kudai kuwa kuna idadi ya wabunge 11 ambao wapo kwenye orodha ya kutekwa na kutolewa uhai na kikundi hicho

“Nimefahamishwa na baaadhi ya mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu na kuna watu wamenitumia ujumbe na kuniambia mimi ni moja kati  wabunge 11 ambao wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai” alisema Bashe wakati anaomba muongozo wa Spika kuhairisha bunge ili kutoa nafasi ya wabunge kujadili juu ya maswala ya utekaji yanayoendelea nchini